Je wajua kuna mipira ya kondomu ya mdomoni?
Nilipokuwa na umri wa miaka 20 shirika moja la wahisani walileta boksi la mipira ya kondomu katika chuo chetu.
Zilisambazwa miongoni mwetu kama maelezo ya kujikinga kiafya, huku tukipigwa na butwaa.
''Wakati ilipofika kwangu nilichukua pakiti moja. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kukumbana na mipira ya kondmu ya mdomoni''.
Njia pekee ya kufikiria kuhusu 'dental dams' ni kuzichukulia kama kondomu za mdomoni.
Zina umbo la mraba na nyengine la mstalili na huwekwa katika uke ama sehemu ya nyuma kwa lengo la kufanya ngono ya kutumia mdomo bila kupitisha maambukizi.
Mara tu mipira hiyo inapowekwa katika maeneo yanayofaa unaweza kuendelea na shughhuli yako huku mipira hiyo ikiwa na ladha tofauti.
Haionekani kuwa mizuri lakini inazuia maambukizi.
Nchini Uingereza , vijana waliopo kati ya umri wa miaka 15-24 wako katika hatari kupatikana na magonjwa yanayosababishwa na ngono STI ikilinganishwa na watu wazima.
Mwaka 2016, vijana kati ya umri wa miaka 15-24 ambayo ni asilimia 62 walipatikana na ugonjwa wa klamidia , asilimia 50 na kisonono, asilimia 49 walikuwa na maambukizi katika sehemu za siri, huku asilimia 42 wakiwa na ugonjwa wa vidonda katika sehemu za siri
Wapenzi wa jinsia moja wako katika hatari ya kuambukizwa na magonjwa ya zinaa.
Ikilinganishwa na ngono kati ya wanawake ambao huonekana kuwa na hatari ya viwango vya chini, huku baadhi ya watu wakidhania kwamba wapenzi wa jinsia moja katika jinsia ya kike na wanawake wanaoshiriki katika mapenzi hayo na wanaume pamoja na wanawake hawako hatarini kupimwa magonjwa hayo ya zinaa.
''Wakati nilipoanza kuwa na mpenzi katika miaka yangu ya ujana sikujua kwamba ngono salama ilikuwa muhimu kwa wapenzi wa jinsia moja hususan wasagaji''.
''Wapenzi wangu wa kwanza walikuwa pia hawajui kwa hivyo hatukutumia kinga yoyote'' .
''Lakini mpira huo wa kondomu wa mdomoni ulinifanya kugundua kwamba wasagaji pia ni muhimu kufanya ngono salama sawa na mtu yeyote yule''.
Kama mipira ya kondomu, mipira hiyo ya Dental Dams inaweza kuharibiwa na huuzwa katika pakiti.
Lakini kama kondomu sio rahisi kununua.
Zinaweza kupatikana katika maduka ya kuuza dawa na hununuliwa mitandaoni.
Kila mtu anaelewa kuhusu mipira ya kondomu na dawa za kuzuia mimba , Zote tulifunzwa shuleni.Lakini kondomu za mdomoni haziangaliliki.Ni wazi kwamba uingiliaji katika sehemu ya uke sio lazima ishirikishe uume katika wasagaji ama wanandoa.
Kuna hatari ya kusababisha maambukizi kupitia uingiliaji wa kidijitali hususan kama mtu ana kidonda ama mkwaruzo katika mkono na iwapo una kidonda na ulikigusa kabla ya kufanya ngono.
Labels: GUMZO MTANDAONI, JE WAJUA?, SOCIAL MEDIA
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home