Sunday 29 October 2017

USHIKAMANA NA MAKAHABA CHANZO CHA UMASKINI part 02

Mpendwa msomaji, Ninafuraha kuu kukutana nawe tena siku hii ya leo tukiendelea sehemu ya pili ya somo letu.Ni mimi Ev. Zachary John Bequeker - Mwanza Tanzania.


Tulijifunza juu ya ukahaba. Tukaangalia maana ya ukahaba, Maana ya kahaba, Namna ukahaba unavyofanyika, Mavazi ya kikahaba na Madhara yake.

Kama hujafanikiwa kusoma sehemu ya kwanza ya somo hili bonyeza hapa chini

Tunasoma katika kitabu cha MITHALI 29:3 "Apendaye hekima humfurahisha babaye; Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali."


Kushikamana na makahaba ni kitendo cha kuwa nao na kuutumia muda kwa pamoja"A Companion of harlots"

Ni dhahiri kuwa, Unapotumia muda wako kuwa na kahaba kuna gharama zinazohitajika.
Inahitajika umuhudumie kwa chakula, ulipie chumba au gharama ya mahali pa kutumia muda wenu pamoja.

Jaribu kuwaza kwa mfano wewe una kipato cha Tsh. 300,000/= kwa mwezi, ambayo ni wastani wa Tsh 10,000/= kwa siku. Jiulize Je, Tsh 10,000/= inatosheleza kumhudumia kahaba,kulipia chumba na gharama zingine?  

Jibu ni la! Haiwezi kujitosheleza. Na matokeo yake ni nini? Matokeo yake itakuwa unahangaika kila siku kutafuta pesa, Pesa unapata lakini hautaona hatua zozote za maendeleo kwa sababu unachota maji na kuyatia ndani ya tenga.

Hata kama ungalikuwa unampatia Tsh 2,000/= kwa siku bado ni nyingi sana. Chukua 2000 x 30 = 60,000/= na ukizidisha kwa miezi 12 unapata ni 720,000/= 

Watu wengi walio rudi nyuma kimaendeleo chanzo ni makahaba. Uliza watakuambia na hata hivyo wewe mwenyewe ni shahidi wa jinsi makahaba wanavyokwamisha mipango yako au walivyokuwa wakikwamisha mipango yako.

Wakati mwingine kuna kuambukizwa magonjwa ya zinaa, badala ya kufanya shughuli za kimaendeleo unaanza kuhangaika kutafuta tiba ya magonjwa hayo. na tiba si bure! bali ni gharama zinahitajika ambazo ni pesa, muda n.k.

Hebu badilika sasa.Achana na tamaa za ukahaba.Hebu tosheka na mme au mke uliyenaye.
UTABADILI BUCHA LAKINI NYAMA NI ILEILE Ikimbie zinaa mara moja sasa 1 KOR 6:18
  Tumeambiwa "Mme mmoja,Mke mmoja" na si vinginevyo  1 KOR 7;2

Kama hujaoa wala kuolewa subiri muda ukifika uataoa au kuolewa. Mwombe Mungu atakupatia unayemhitaji kwani Mungu anakuuliza unataka nikufanyie nini? Mwambie Mungu nataka unipe mke au Mungu nataka unipe mume.

UKO TAYARI KUONDOLEWA KIU YA UKAHABA ?
Naamini uko tayari. Fuatisha maneno haya kwa dhati ya moyo wako na baada tu ya kumaliza uataona badiliko katika masha yako.

SEMA   " Mungu Baba, Mimi ni mchafu mbele zako, Nimekutenda dhambi kwa namna ya kutisha, Lakini sasa naja mbele zako nikihitaji msamaha. Nakuomba Bwana ufute jina langu katika vitabu vya hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima wa milele. Mungu ondoa kiu ya ukahaba ndani yangu kuanzia sasa niwe mtoto wako. Sitaki ukahaba tena. Nipe roho ya kutosheka na mke/mme niliyenaye Katika jina la YESU AMEN!" 
Sasa umeokoka , hamu ya ukahaba haipo tena.

Tafuta mahali penye kanisa linalohubiri wokovu kwa msaada zaidi na Mungu akubariki.
WASILIANA NAMI KWA 0758 590 489/ 0625 966 236




Share on Google Plus

MSIMAMIZI WA BLOG HII

Mimi ni mwinjilisti Zachary John Bequeker toka Mwanza Tanzania. Karibuni tujifunze neno la Mungu pamoja.
pia waweza pata masomo ya neno la Mungu Youtube kwa kuandika Zachary Bequeker au ZAKACHEKA.
0625 966/ 0758 590489

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home